Search Box

Friday, May 16, 2014

Hatimaye Jay Z, Beyonce na Solange wavunja ukimya

Hatimaye Jay Z, Beyonce na mdogo wake Solange wametoa tamko rasmi kuhusu ugomvi uliotokea kwenye lift na video yake kusambaa kwenye mitandao ikimuonesha Solange akimpiga makofi na mateke Jay Z.
Watatu hao waliandika tamko lao na kulituma kwa Associated Press, May 15.
Wanafamilia hao kwa pamoja wameeleza katika tamko lao kuwa wameyamaliza matatizo yote kama wanafamilia na kwamba ni kawaida kwa familia zote kugombana na wao ni sehemu ya familia hizo pia.
“Kutokana na press release iliyotolewa ya video ya tukio lilitokea kwenye lift kuanzia Jumatatu, May 5, kumekuwa na usambaaji mkubwa wa maelezo kuhusu nini kilisababisha tukio hilo. Lakini kitu cha muhimu zaidi ni kwamba familia yetu imeshalishughulikia na limeisha.
“Jay na Solange kila mmoja amechukua jukumu lake kwa kile kichotokea. Wote wametambua nafasi yao waliyohusika katika hili suala la faragha ambalo limetolewa hadharani. Wote wameombana msamaha na tunaendelea mbele kama familia iliyoungana.” Wameandika katika tamko hilo.
Hata hivyo wamekanusha ripoti zilizoeleza kuwa katika siku hiyo Solange na alikuwa amelewa sana na kwamba muda wote alikuwa akionesha tabia sizizo za heshima.
“Mwisho wa siku familia zote zina matatizo na sisi hatuko tofauti. Tunapendana na zaidi ya yote sisi ni familia. Tumeliweka hili nyuma na tunatumaini mtu mwingine yeyote pia atafanya hivyo pia.”
Bado tetesi za chanzo cha ugomvi wao zinaelezwa kuwa ni kitendo cha Jay Z kuonekana anakuwa na ukaribu sana na mwanamitindo Rachel Roy kitu ambacho hakikuwafurahisha Beyonce na Solange.
Chanzo kimeliambia New York Daily News kuwa kitu kilichopandisha hasira za Solange zaidi ni pale Jay Z alipotaka kwenda kwenye after party ya Rihanna bila Beyonce na ikaonekana kama ataenda na Rachel Roy.

HIT: JCB ft FiD Q & KalaPina (@karamamasoud) – Sina Muda

JCB_FID_KALAPINA_500 
JCB (@jcb_makalla) Ft Fid Q (@FidQ) & Kalapina (@karamamasoud)
Ngoma ni HipHop Category juu ya Beat toka kwa Producer Black Muslim wa NorthBlock Records Arusha na Vocal Mixing amesimamia Ben Mwamba, Kwa Mahojiano/Mazungumzo zaidi check na JCB kupitia Whatsapp Number +45 527 500 60

HIT: Linex - ONGA ONGA

http://photos-h.ak.instagram.com/hphotos-ak-prn/10299857_705234936186255_1427808804_n.jpg
Linex ametoa wimbo mpya kabisa ambao yeye mwenyewe anasema kuwa wimbo huu ndio official (yaani rasmi) kwa mwaka huu. Mwezi mmoja nyuma zilitoka nyimbo zake ambazo yeye mwenyewe linex amesema hakuzitoa ila zilivuja kwa bahati mbaya, kwahiyo kwa mwaka huu wimbo huu “onga onga” ndio wimbo wake wa kwanza kutoa. Wimbo umefanyikia pale Sharobaro records chini ya usimamizi wa producer ambaye huwa anafanya kazi zake kwa umakini mkubwa huyu si mwingine ni bob junior. Ebu sikiliza huu wimbo unavyochezeka.

Wimbo                :         Honga Honga
                                         Msanii                 :         Linex
             Studio                  ;         Sharobaro Records
Producer             :         Bob Junior
                                        Contact za linex        :         0713 991149

Thursday, May 1, 2014

PHOTOS: Uzinduzi wa Video ya Gere kutoka kwa Weusi

Kundi la Weusi linaloundwa na rappers kutoka Arusha, Joh Makini, Nick wa Pili, G-Nako na Bonta jana usiku (April 30) walizindua video ya wimbo wao unaofanya vizuri hivi sasa ‘Gere’ kwenye hotel ya Meditteraneo iliyopo jijini Dar es Salaam

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki na wasanii wenzao na wadau wa muziki nchini







 

© 2013 Bongo Muzik. All rights resevered. Designed by Samber Junior

Back To Top