Na Katuma Masamba
BILA shaka jina Maro Protas ni jipya
miongoni mwa masikio ya walio wengi, na hii ni kutokana na wengi wetu
kutofuatilia muziki wa asili ya Kitanzania.
Maro ni mwanamuziki na mchezaji wa ngoma
za asili ambapo ni kijana kutoka katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa sasa
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Tasuba), ambapo kupitia kazi yake hiyo
ameweza kulitangaza taifa letu ipasavyo.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya
Maro anasema tasnia hiyo ya ngoma za asili bado Watanzania wengi wanaonekana
kutoielewa na kuchukulia kama ni kitu ambacho hakina maana yoyote bila kujua
kama ni asili yao.
Anasema tasnia hiyo inahitaji kupewa
kipaumbele kama zilivyo tasnia nyingine za mpira, muziki wa kizazi kipya na
nyinginezo, ngoma za asili ni utamaduni wa Afrika na Tanzania kwa ujumla hivyo
tasnia hiyo ina uwezo wa kuitangaza nchi kuliko tasnia nyingine.
Maro anawashangaa Watanzania na
hususani vijana wanaopenda utamaduni wa nchi za Magharibi na kusema ni moja
kati ya sababu zinazofanya vijana wa sasa kukosa heshima kutokana na kuwa na
utamaduni ambao sio wa kwao.
“Katika tasnia hii wapo watu ambao
wanaielewa na wanaipenda kutokanana kuwa ndiyo utamaduni wao, lakini wapo
wengine wanaodharau utamaduni wetu na ndiyo maana hata watoto wa siku hizio
wanaporomoka kimaadili.
"Unakuta familia nzima asubuhi
wanasalimiana kingereza tu, hata lugha yao nyumbani kwao hajui kuiongea unategemea
watoto wao watafanya nini?, ila kwa waelewa ukiwa unazungumza nao unajisikia
fahari leo hii mwambie mtoto akuimbie wimbo wowote ule wa asili kama ataweza lakini
sasa mwambie niimbie wimbo wa kingereza ataimba
haraka" alisema Protas.
Aliongeza "yatupasa kujivunia
utamaduni wetu na tuachana na huu ukoloni mambo leo kuna vikundi vingi vya
sanaa, ambapo kwa sasa unaweza ukaona kuna baadhi ya vijana wamepata muamko na
kujiunga" alisema.
Anasema wasanii wa kizazi kipya
wamekuwa wakiendekeza zaidi utamaduni wa Magharibi na kusahau kuutangaza
utamaduni wa Tanzania pia kusahau wao ni kioo cha jamii hivyo baadhi ya watu
kuiga kile wanachofanya wao ikiwa ni pamoja kuiga vitendo vya hovyo
vinavyofanywa na wasanii hao.
Aidha Protas alisema kuwa wakati
mwingine utamaduni huo wa Kimagharibi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa
kuporomoka kwa maadili ya taifa,"Unajua hata sasa hivi ukiangalia tabia za
vijana wengi zimekuwa ni mbovu kupindukia, si ajabu kijana kutoa matusi ya
ajabu mbele ya wazee," aliongeza Protas.
Maro anaeleza kuwa wasanii wa tasnia
hiyo hamna faida wanayopata zaidi ya umaarufu, kutokana na malipo hafifu ambayo
hulipwa kutokana na maonyesho wanayoyafanya jambao ambalo hufanya baadhi yao
wanapostaafu kuishi katika mazingira magumu.
Protas ameishauri serikali kuhakikisha
tasnia hiyo inakuwa
nilianzia shule kuimba imba nikiwa sekondari
mwaka 2003 nikiwa songe sec baada ya hapo niliamia ellys sec bunda mwaka 2005
mpka 2007 mpaka kumaliza masomo yangu ya sec nikiwa ellys nilikuwa mwenyekiti
wa burudani baada ya hapo nilijiunga na chuo cha sanaa bagamoyo kwa sasa ni
taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo (tasuba) mwaka 2008 mpka 211 kwa
kuongeza elimu ya sanaa ya fani ya muziki wa asili pamoja na uchezaji ngoma za
asili nikiwa tasuba nilifanikiwa kwenda nchi tofauti tofauti kushiriki katika
matamasha mbalimbali kuiwakilisha nchi na pia kuutangaza utamaduni wa taifa
langu 2009 mwezi wa kumi na moja nilishiliki katika tamasha la umoja cultural
flaying carpet nchini ethiopia tamasha linalowakutanisha wasanii 100 kutoka
nchi za tanzania kenya uganda ethiopia nethaland na norwey mwaka 2010 mwezi wa
sita nilienda shanghai china kwenye tamasha liitwalo expo lenye madhumuni ya
kibiashara za kitamaduni kila nchi dunia kote zilishiliki mwezi wa 10 mwaka huo
huo nilienda nethaland na norwey kwenye program itwayo nota exchange tanzania
na norwey 2012 nilienda kenya na uganda pia kenye tamasha la kujitilea festival
matamasha ya ndani niliyoshiliki ni pamoja na ziff zanzibar international filim
festival sauti za busara yote haya hufanyika zanzibar, bagamoyo festival na
matamasha mengine mbali mbali pamoja na show za kawaida baadhi ya mikoa ya
tanzania kama dar es salaam morogoro pwani arusha dodoma singida mwanza mara nk
mafanikio yapo tukisafili tunalipwa ujira ambao unakufanya uweze kuishi
vizuriiiiiiiiiiiii.
tasnia ta ngoma za asili kuna watu
wenye uelewa na hiki kitu na kuna watu ambao wao hudharau asili yetu na
kujikuta wakikopi vya ulaya kila kukicha na ndiyo maana watoto wa sku hizi
huporomoka kimaadili ni kwwa sababu unakuta famlia nzia wanasalimiana
kiingereza hawajua hata lugha yao unategemea watoto wao watafanya nn ila kwa
waelewa ukiwa unazungumza nao hadi unajsikia fahari leo hii mwambie mtoto
akuimbie wimbo wowote ule wa asili kama anaweza ila mwambie niimbie wimbo wa
kizungu haraka haraka kiukweli yatupasa kujivinia cha kwetu na tuachana na huu
ukoroni mambo leo kuna vikundi vingi sana kwa sasa nchini na vijana wameanza
kuamka nashukuru kwa hilo serikali kwanza ukiangalia bunge naamini katika
wizara inayopewa bajeti ndogo wizara ya habari vijana michezo na utamaduni nayo
pia ni miongoni mwa hizo tunakuaga maarufu sana katika sherehe zao za
kiserikali kwa huko mikoani wanatutumia kwa ujira mdogo sana na kutuacha
hivyohivyo kwa dar es salaam watu walisha anza kustuka bei watakayo chukulia
band ya muzki wa kisasa au msanii wa bongo flava ni tifauti na bie atakayo
chukuliwa msanii wa ngoma za asili hivyo serikali ingepanga viwango vya bei za
wasanii katika kila ngazi mkoa kwa mkoa taifa kwa taifa chuo cha sanaa bagamoyo
kina kufa serikali inakiangalia wasomeshe wasanii wawe na elimu ya sanaa ya darasani
na ya jukwaani usha uri kwa wasanii wengine tuwe na nidhamu katika kazi
tujeshimu na si tutaheshimiwa tuwe wa bunifu na tupate fulsa ya kwenda mkoani
kujifunza ngoma mbali mbali siyo kuchezea uzoefu tu hapo tutafanikiwa kwa wale
wanaojua sanaangoma za asli siyo dili imekula kwao sanahii inafursa kubwa sana
na ndiyo azina ya nchi mfano kaja obama hukuona bongo flava hata 1 walikuwepo
wasanii wa ngoma hii ni wazi tujivunie cha kwetu nao wazipende nyimbo za kwao