Search Box

Monday, February 17, 2014

MARO; MSANII WA ASILI ANAYELILIA HESHIMA YA MUZIKI

5:56 AM



 Na Katuma Masamba
BILA shaka jina Maro Protas ni jipya miongoni mwa masikio ya walio wengi, na hii ni kutokana na wengi wetu kutofuatilia muziki wa asili ya Kitanzania.
Maro ni mwanamuziki na mchezaji wa ngoma za asili ambapo ni kijana kutoka katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa sasa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Tasuba), ambapo kupitia kazi yake hiyo ameweza kulitangaza taifa letu ipasavyo.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya Maro anasema tasnia hiyo ya ngoma za asili bado Watanzania wengi wanaonekana kutoielewa na kuchukulia kama ni kitu ambacho hakina maana yoyote bila kujua kama ni asili yao.
Anasema tasnia hiyo inahitaji kupewa kipaumbele kama zilivyo tasnia nyingine za mpira, muziki wa kizazi kipya na nyinginezo, ngoma za asili ni utamaduni wa Afrika na Tanzania kwa ujumla hivyo tasnia hiyo ina uwezo wa kuitangaza nchi kuliko tasnia nyingine.
Maro anawashangaa Watanzania na hususani vijana wanaopenda utamaduni wa nchi za Magharibi na kusema ni moja kati ya sababu zinazofanya vijana wa sasa kukosa heshima kutokana na kuwa na utamaduni ambao sio wa kwao.
“Katika tasnia hii wapo watu ambao wanaielewa na wanaipenda kutokanana kuwa ndiyo utamaduni wao, lakini wapo wengine wanaodharau utamaduni wetu na ndiyo maana hata watoto wa siku hizio wanaporomoka kimaadili.
"Unakuta familia nzima asubuhi wanasalimiana kingereza tu, hata lugha yao nyumbani kwao hajui kuiongea unategemea watoto wao watafanya nini?, ila kwa waelewa ukiwa unazungumza nao unajisikia fahari leo hii mwambie mtoto akuimbie wimbo wowote ule wa asili kama ataweza lakini sasa mwambie niimbie wimbo wa kingereza ataimba  haraka" alisema Protas.
Aliongeza "yatupasa kujivunia utamaduni wetu na tuachana na huu ukoloni mambo leo kuna vikundi vingi vya sanaa, ambapo kwa sasa unaweza ukaona kuna baadhi ya vijana wamepata muamko na kujiunga" alisema.
Anasema wasanii wa kizazi kipya wamekuwa wakiendekeza zaidi utamaduni wa Magharibi na kusahau kuutangaza utamaduni wa Tanzania pia kusahau wao ni kioo cha jamii hivyo baadhi ya watu kuiga kile wanachofanya wao ikiwa ni pamoja kuiga vitendo vya hovyo vinavyofanywa na wasanii hao.
Aidha Protas alisema kuwa wakati mwingine utamaduni huo wa Kimagharibi umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili ya taifa,"Unajua hata sasa hivi ukiangalia tabia za vijana wengi zimekuwa ni mbovu kupindukia, si ajabu kijana kutoa matusi ya ajabu mbele ya wazee," aliongeza Protas.
Maro anaeleza kuwa wasanii wa tasnia hiyo hamna faida wanayopata zaidi ya umaarufu, kutokana na malipo hafifu ambayo hulipwa kutokana na maonyesho wanayoyafanya jambao ambalo hufanya baadhi yao wanapostaafu kuishi katika mazingira magumu.
Protas ameishauri serikali kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa

nilianzia shule kuimba imba nikiwa sekondari mwaka 2003 nikiwa songe sec baada ya hapo niliamia ellys sec bunda mwaka 2005 mpka 2007 mpaka kumaliza masomo yangu ya sec nikiwa ellys nilikuwa mwenyekiti wa burudani baada ya hapo nilijiunga na chuo cha sanaa bagamoyo kwa sasa ni taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo (tasuba) mwaka 2008 mpka 211 kwa kuongeza elimu ya sanaa ya fani ya muziki wa asili pamoja na uchezaji ngoma za asili nikiwa tasuba nilifanikiwa kwenda nchi tofauti tofauti kushiriki katika matamasha mbalimbali kuiwakilisha nchi na pia kuutangaza utamaduni wa taifa langu 2009 mwezi wa kumi na moja nilishiliki katika tamasha la umoja cultural flaying carpet nchini ethiopia tamasha linalowakutanisha wasanii 100 kutoka nchi za tanzania kenya uganda ethiopia nethaland na norwey mwaka 2010 mwezi wa sita nilienda shanghai china kwenye tamasha liitwalo expo lenye madhumuni ya kibiashara za kitamaduni kila nchi dunia kote zilishiliki mwezi wa 10 mwaka huo huo nilienda nethaland na norwey kwenye program itwayo nota exchange tanzania na norwey 2012 nilienda kenya na uganda pia kenye tamasha la kujitilea festival matamasha ya ndani niliyoshiliki ni pamoja na ziff zanzibar international filim festival sauti za busara yote haya hufanyika zanzibar, bagamoyo festival na matamasha mengine mbali mbali pamoja na show za kawaida baadhi ya mikoa ya tanzania kama dar es salaam morogoro pwani arusha dodoma singida mwanza mara nk mafanikio yapo tukisafili tunalipwa ujira ambao unakufanya uweze kuishi vizuriiiiiiiiiiiii.
tasnia ta ngoma za asili kuna watu wenye uelewa na hiki kitu na kuna watu ambao wao hudharau asili yetu na kujikuta wakikopi vya ulaya kila kukicha na ndiyo maana watoto wa sku hizi huporomoka kimaadili ni kwwa sababu unakuta famlia nzia wanasalimiana kiingereza hawajua hata lugha yao unategemea watoto wao watafanya nn ila kwa waelewa ukiwa unazungumza nao hadi unajsikia fahari leo hii mwambie mtoto akuimbie wimbo wowote ule wa asili kama anaweza ila mwambie niimbie wimbo wa kizungu haraka haraka kiukweli yatupasa kujivinia cha kwetu na tuachana na huu ukoroni mambo leo kuna vikundi vingi sana kwa sasa nchini na vijana wameanza kuamka nashukuru kwa hilo serikali kwanza ukiangalia bunge naamini katika wizara inayopewa bajeti ndogo wizara ya habari vijana michezo na utamaduni nayo pia ni miongoni mwa hizo tunakuaga maarufu sana katika sherehe zao za kiserikali kwa huko mikoani wanatutumia kwa ujira mdogo sana na kutuacha hivyohivyo kwa dar es salaam watu walisha anza kustuka bei watakayo chukulia band ya muzki wa kisasa au msanii wa bongo flava ni tifauti na bie atakayo chukuliwa msanii wa ngoma za asili hivyo serikali ingepanga viwango vya bei za wasanii katika kila ngazi mkoa kwa mkoa taifa kwa taifa chuo cha sanaa bagamoyo kina kufa serikali inakiangalia wasomeshe wasanii wawe na elimu ya sanaa ya darasani na ya jukwaani usha uri kwa wasanii wengine tuwe na nidhamu katika kazi tujeshimu na si tutaheshimiwa tuwe wa bunifu na tupate fulsa ya kwenda mkoani kujifunza ngoma mbali mbali siyo kuchezea uzoefu tu hapo tutafanikiwa kwa wale wanaojua sanaangoma za asli siyo dili imekula kwao sanahii inafursa kubwa sana na ndiyo azina ya nchi mfano kaja obama hukuona bongo flava hata 1 walikuwepo wasanii wa ngoma hii ni wazi tujivunie cha kwetu nao wazipende nyimbo za kwao

Written by

We are Creative Blogger Theme Wavers which provides user friendly, effective and easy to use themes. Each support has free and providing HD support screen casting.

0 comments:

Post a Comment

 

© 2013 Bongo Muzik. All rights resevered. Designed by Samber Junior

Back To Top