Positive Music for the people ni mradi (Project) ulio chini Stopa The
Rhymecca a.k.a Yokoi mradi huo ukiwa na lengo la kuelimisha jamii
kupitia muziki katika mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakigusa jamii
kwa njia mbalimbali kijamii, kisiasa na kiuchumi. Zimeshuhudiwa nyimbo
nyingi za kuparty, kusema unamiliki gun au benz lakini sio kweli,
unampenda binti ambae uwezo wako hamuendani, kujisifu mimi mkali kuliko
flani na mabo mengine je mwisho wa siku unaifundisha nini jamii yako
iliyo maskini yenye kuhitaji elimu ili kukabili maisha maisha magumu
yanayowakabili kila siku? Takwimu inaonyesha wengi wanaopenda muziki wa
bongo falava ni maskini kitu kinachopelekea hata muziki wetu kutofanya
vizuri sana kutokana na mashabiki kutonunua bidhaa za wasanii kikamilifu
kutokana na umasikini wao. Mradi wa Positive Music for the People
itakuwa inajumuisha nyimbo zenye kuelimisha jamii katika nyanja
mbalimbali kutunza mazingira, ajali za barabarani, kujikinga na ukimwi,
wanafunzi kuzingatia masomo kwani hakuna njia nyingine ya kuwasaidia
zaidi ya kupata elimu, madhara ya pombe, rushwa na mambo mengine muhimu
ili mradi kuelimsiha jamii. Katika mradi huu ilishatoka ngoma ya ajali
za barabarani inayoitwa “Ajali” ikafuatiwa na “Punguza Mwendo” amabazo
zilikuwa zimedhaminiwa na Road Safety Council of Tanzania kusaidia
kufanya video na mambo mengine. Kwa sasa kutoka mradi wa Positive Music
for the People imetoka ngoma inayohimiza kupiga vita uharamia wimbo
unaitwa “Save the elephants and rhinos” iliyotengenezwa na Ben Mwamba
kwenye studio za Mpo Africa Dar es salaam. Akizungumza Stopa Yokoi
amesema album ya Positive Music for the People inataarajiwa kukamilika
katika mwa mwaka huu wa 2014

0 comments:
Post a Comment